TANGAZO
TANZANIA ASSOCIATION OF MICROFINANCE INSTITUTIONS (TAMFI)
P. O. BOX 19798 DAR ES SALAAM
Email: dcb@africaonline.co.tz;
Website: www.tamfi.com
WITO WA KUJIUNGA NA TAMFI – WANACHAMA WAPYA
Bodi ya Wakurugenzi wa TAMFI inapenda kuwaarifu na kuwaalika wadau wa Asasi zinazotoa huduma za kifedha kwa watu wenye kufanya shughuli ndogondogo na za kati (Mirofinance) kujiunga na mtandao huu wa TAMFI. TAMFI ni kwa ajili ya Taassi zote zilizoko Mijini na Vijijini. Wasiliana nasi kwa kutumia namba za simu au barua pepe zilizotajwa hapo chini..
UTANGULIZI
TAMFI ni Shirika la mtando wa kitaifa wa Asasi zinazojihusisha na utoaji wa huduma za kifedha kwa watu wenye kufanya shughuli ndogo ndogo na za kati na taasisi zinazojihusisha na utoaji wa huduma mbalimbali kwa Asasi hizo za fedha. Makao makuu ya Shirika la Mtandao huu yapo Jijini Dar es Salaam katika Jengo la biashara ndogondogo la SIDO liliko katika barabara ya Bibi Titi Mohamed chumba na 25 na 26 upande A.
FAIDA ZA KUWA MWANACHAMA WA TAMFI
Ukiwa mwanachama wa TAMFI unategemea kupata faida zifuatazo:
Kupata fursa ya kushirikiana kwa karibu na Asasi nyingine za Kitanzania na za Kimataifa.
Kupata fursa ya kujitangaza kupitia mtandao wa chama, tovuti ya chama, majarida ya chama na katika matukio na shughuli mbalimbali za mtandao..
Kupata fursa ya kushiriki katika mafunzo adimu kwa gharama nafuu.
Kupata fursa ya kuhabarishwa kwa taarifa au habari muhimu za sekta kutoka ndani na nje ya nchi.
Kupata fursa ya kuunganishwa na wafadhili, wahisani na taasisi mbalimbali za kifedha na huduma nyinginezo kutoka ndani na nje ya nchi.
Kunufaika na nguvu kubwa ya pamoja katika kutatua matatizo yanayoikabili Sekta katika ngazi mbalimbali.
Kunufaika na nguvu kubwa ya kusemewa Kisekta katika vyombo vya Serikali na vya Kimataifa.
Mawasiliano:
Kwa wanaohitaji kujiunga na TAMFI wanaombwa kuwasiliana na watu wafuatao ili kuweza kupata fomu za maombi na maelezo ya ziada:
i. Edmund Mkwawa (Mwenyekiti) Simu Na. 0754 284831, Barua pepe: eddymkwawa@yahoo.co.uk; dcb@africaonline.co.tz,
ii. Joel Mwakitalu (Makamu Mwenyekiti) Simu Na. 0784 657718, Barua pepe: joelmwakitalu@yahoo.com,
WOTE MNAKARIBISHWA TUJENGE TAIFA LETU KWA NGUVU YA UMOJA
Jovin Marco Ndungi
K.n.y: KATIBU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment